Tusipokuwa na imani, hali zinazotuzunguka zinaendelea kwenda
katika mwelekeo mbaya, lakini tunapokuwa na imani,
kila kitu huenda vizuri.
Ni lazima tutambue kanuni hii kupitia Biblia
na tutupilie mbali wasiwasi, hofu, mashaka na
fadhaa zetu zote katika maisha yetu ya imani.
Biblia inarekodi kazi ya Gideoni,
kazi ya Yoshua, kazi ya kugawanya Bahari
ya Shamu, na kazi ya mikate mitano
ya shayiri na samaki wawili.
Ilionekana kuwa haiwezekani kwa macho ya kimwili,
lakini Mungu Alifanikisha kila kitu.
Vivyo hivyo, tukiamini maneno ya Kristo Ahnsahnghong
na Mungu Mama na mafundisho ya Yesu
kwamba injili ya agano jipya itahubiriwa kwa
ulimwengu wote, kila kitu kitatimizwa
kulingana na maneno Yao.
Lakini kama mtu ana shaka kuhusu kile
anachokula, amehukumiwa, kwa sababu hakula kwa imani.
Kwa kuwa chochote kinachofanywa pasipo imani ni dhambi.
Warumi 14:23
Yesu akamwambia, “Kama ukiweza kuamini,
yote yawezekana kwake yeye aaminiye.”
Marko 9:23
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha