Baadhi ya watu huchukulia Biblia
kama kitabu cha historia au hekaya za Israeli tu.
Walakini, Biblia ni kitabu kongwe zaidi ulimwenguni,
kilichoandikwa kwa nyakati tofauti na makumi ya watu
wa kazi na umri tofauti zaidi ya miaka 1,600.
Kinachoshangaza zaidi ni kwamba mambo yote
yaliyoandikwa kwa zaidi ya miaka 1,600
yameunganishwa kama unabii na utimizaji.
Miongoni mwa rekodi za Biblia,
tujifunze unabii kuhusu Mfalme Koreshi
na utimizaji wake.
Mfalme Koreshi alikuwa mwanzilishi wa Milki ya Uajemi
na mshindi wa Mashariki.
Tuangalie mafanikio yake makubwa
yaliyoandikwa katika Biblia.
“Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi: “ ‘ BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote duniani, na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda.Ezr 1:2–3
Kwa nini Koreshi, mfalme wa Uajemi,
alimsifu Mungu wa Israeli na kuwaweka Waisraeli huru?
Mfalme Koreshi aliona jina lake likiandikwa katika kitabu cha Isaya
ambacho kilikuwa kimeandikwa takribani miaka 170
kabla hajawaweka huru Waisraeli.
“Hili ndilo asemalo BWANA kwa mpakwa mafuta wake,
Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume
kutiisha mataifa mbele yake . . . Nitakupa hazina za gizani,
mali zilizofichwa mahali pa siri, ili upate kujua ya kwamba Mimi ndimi BWANA,
Mungu wa Israeli, akuitaye kwa jina lako.” Isa 45:1–3
Mfalme Koreshi alikuja kutambua kwamba Mungu
Alimsaidia kushinda Babeli, naye akawaweka huru
Waisraeli kama ilivyotabiriwa katika Biblia.
Matokeo yake, Mfalme Koreshi bado amesifiwa na watu kama mfalme wa kale
aliyewaweka watumwa huru na kutambua haki ya uhuru wa dini.
Biblia pia ilitabiri kuzaliwa kwa Yesu kama mtoto takribani
miaka 700 kabla ya kuja Kwake duniani.
. . . Bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana,
na ataitwa Imanueli. Isa 7:14
Kulingana na unabii huu, Mungu Alizaliwa kama Yesu
kupitia mwili wa bikira Maria (Mt 1:18–23).
Zaidi ya hayo, Biblia ilitabiri kwa undani jinsi Yesu Atakavyoteseka.
Alidharauliwa na kukataliwa
na wanadamu, . . . Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu,
alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu;
adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake,
na kwa majeraha yake sisi tumepona.
Isa 53:3–5
Kulingana na unabii huu, Yesu Alichomwa kwa mkuki
na kupigwa mijeledi (Mt 27:26–35; Yoh 19:34).
Ijapokuwa unabii wa Biblia haukueleweka
na watu ulipoandikwa, wote umetimizwa.
Hivyo Biblia inatuonya tusidharau
maneno ya unabii (1 The 5:20).
Ni kwa sababu hatuwezi kuokolewa
ikiwa tunaudharau unabii wa Biblia.
Kwa kuwa unabii mwingi umetimizwa hasa kama ilivyoandikwa,
vivyo hivyo unabii uliobaki utatimizwa bila kushindwa.
Kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi,
na njaa kali, na magonjwa ya kuambukiza katika sehemu mbalimbali.
Pia kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni. Lk 21:11
Biblia inatuambia kwamba lazima tukimbilie Sayuni
ili kuokolewa maafa na maangamizi makuu ya mwisho yanapokuja.
“. . . ‘Kusanyikeni pamoja! . . . Onyesheni ishara ili kwenda Sayuni!
Kimbilieni usalama pasipo kuchelewa!
Kwa kuwa ninaleta maafa kutoka kaskazini, maangamizi ya kutisha.” Yer 4:5-6
Sayuni, mahali ambapo sikukuu za Mungu huadhimishwa,
ni mahali pa makimbilio na wokovu Mungu Ametuahidi (Isa 33:20).
Ulimwenguni, Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu
ndilo kanisa pekee linaloadhimisha sikukuu za Mungu
kulingana na mafundisho ya Biblia; ni Sayuni.
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha