Kupitia tukio la kihistoria kwamba Yesu Alipaa Mbinguni miaka 2,000 iliyopita, Mungu Ametupa tumaini la kupaa–tumaini lililo hai kwamba tutabadilishwa kwa uweza wa Mungu na kumlaki Bwana hewani.
Enoki alitembea na Mungu sikuzote, naye akaenda juu Mbinguni akiwa hai,
akikubaliwa kuwa mtu aliyempendeza Mungu.
Noa pia alitembea na Mungu kila wakati, na aliokolewa kutoka hukumu ya maji.
Elisha alimfuata Eliya hadi mwisho kabisa— hadi ile siku Eliya aliyopaa Mbinguni,
naye akawa nabii baada yake.
Leo, waumini wa Kanisa la Mungu wanaishi maisha ya toba yanayompendeza Mungu,
kwa kutembea na Baba Ahnsahnghong na Mungu Mama katika njia ya Injili
wakiwa na tumaini la kupaa.
Kwa imani Enoki alitwaliwa kutoka maisha haya, kiasi kwamba hakuonja mauti . . .
alikuwa ameshuhudiwa kuwa ni mtu aliyempendeza Mungu. Waebrania 11:5
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha