Kitabu hiki kinasema sehemu ya kimafumbo zaidi ni Mwanzo, ambapo Mungu Ametajwa kama “tu-“.
Wakati Mungu Baba Alipomuumba mtu, hakusema, “Nifanye mtu …,” bali Alisema, “Tufanye mtu …” (Mwanzo 1:26)
Mungu ni mmoja, ambaye ni “Baba”! Hivyo basi, kwa nini Mungu Amefafanuliwa kama “tu-” katika Biblia?
“Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.”Mwanzo 1:1
Katika Torati, maandishi ya awali ya Biblia, imeandikwa kama Elohim ambayo maana yake ni Mungu katika wingi.
Elohim maana yake ni Mungu katika wingi kama hali ya wingi ya El au Eloah maneno yanayomaanisha Mungu katika umoja.
Katika Biblia, neno Mungu limeandikwa katika hali ya wingi [Elohim] zaidi ya mara 2,500. Hii inaonyesha kwamba lazima kuwepo na Mungu mwingine, sio tu “Mungu Baba.” Mwanaume na mwanamke waliumbwa kwa mfano wa Mungu.
“Mungu [Elohim] alimuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe, kwa mfano wa Mungu [Elohim] alimuumba; mwanaume na mwanamke aliwaumba.” Mwanzo 1:27
Mwanaume aliumbwa kwa mfano wa “Mungu Baba.” Mwanamke aliumbwa kwa mfano wa “Mungu Mama.” “Elohim” yaani Muumba ni Mungu Baba na Mungu Mama.
Na imetabiriwa kwamba Mungu Atatokea katika siku za mwisho. (1Timotheo 6:15)
Katika Enzi ya Mwana, Mungu Alitokea kama Yesu.
Katika enzi hii, Elohim, yaani, Mungu Baba na “Mungu Mama,” Watakuja katika mwili kuwaokoa wanadamu.
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu linawaamini Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama kuwa Roho na Bibi arusi – Waokozi katika Enzi ya Roho Mtakatifu.
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha