Mose alikuwa mfano uliotangulia wa kiunabii wa uhalisi katika Yesu.
Waisraeli walishinda vita huko Refidimu wakati Mose alipoinua mikono yake.
Huu ulikuwa unabii kwamba watu wa Mungu watashinda vita
vya kiroho dhidi ya Shetani wakati Yesu Alipoinuliwa msalabani.
Waisraeli walipoumwa na nyoka wenye sumu
na wengi wao walikufa, Mungu Alisema,
“Tengeneza nyoka na uiweke juu ya mti;
mtu yeyote anayeumwa anaweza kuitazama na kuishi.”
Walakini, walisahau nguvu ya maneno ya Mungu
yaliyowaokoa wakaabudu nyoka ya shaba hata baada ya
miaka 800. Kama matokeo, wakachochea hasira ya Mungu.
Hii ilikuwa kivuli inayoonyesha kwamba watu leo
wataangamizwa kwa kuuabudu msalaba,
wakisahau agano jipya ambalo
Kristo Alilianzisha kupitia dhabihu Yake.
Sio mapenzi ya Mungu kwamba tunaisimamisha misalaba.
Kwa Wakristo wa mapema, msalaba ulikuwa si kitu
ila mti uliolaaniwa ambapo Yesu Alisulubiwa.
“Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu au anatoa sanamu,
kitu chukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi-na kuiweka kwa siri.”
Ndipo watu wote watasema, “Amina!”
Kumbukumbu la Torati 27:15
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha