Tukipanda mema, hakika tutavuna matokeo mazuri, na tukipanda uovu, tutavuna matokeo mabaya.
Ni lazima tukumbuke historia ambapo Waisraeli, waliolalamika jangwani kwa miaka arobaini, waliangamizwa, na kijana Daudi, Shadraki, Meshaki, na Abednego walibarikiwa sana na Mungu kwa kumpa shangwe kupitia maneno yao ya imani yaliyojaa neema.
Kwa mujibu wa mafundisho ya Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama, waumini wa Kanisa la Mungu daima hutoa faraja na msaada kwa njia ya matendo mema na maneno maadilifu nyumbani, Kanisani, na katika jamii.
Leo, wanasonga mbele kwa nguvu ili kushiriki habari za furaha za wokovu wa Mungu na wale ambao wamechoka kutokana na maisha magumu, wakitangaza, “Kuna ufalme wa mbinguni ambapo hakuna mauti wala mateso wala maumivu.”
“Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka hazina ya mambo mema yaliyohifadhiwa ndani yake, naye mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutoka hazina ya mambo maovu yaliyohifadhiwa ndani yake.
Lakini nawaambia, katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu kuhusu kila neno lisilo maana walilonena.
Kwa maana kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.”
Mathayo 12:35–37
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha