Waisraeli walipoondoka Misri, kwanza kabisa Mungu Alidhihirisha nguvu ya Pasaka, na Akatangaza Pasaka kupitia Sheria ya Musa, Akiwaamuru waiadhimishe kwa vizazi vijavyo kwa wakati ulioamriwa.
Baadaye, watu wa Mungu walisifiwa na kulindwa dhidi ya maafa baada ya kuadhimisha Pasaka, naye Yesu pia Aliadhimisha Pasaka Akiwa pamoja na wanafunzi Wake, Akiwapa baraka ya uzima wa milele.
Tangu Pasaka ilipoondolewa mnamo mwaka 325 BK, makanisa yote yamekuwa yakishika desturi za mungu wa kipagani.
Walakini, waumini wa Kanisa la Mungu hutambua umuhimu wa Pasaka, ambayo Mungu Aliwaamuru watu Wake waiadhimishe kwa vizazi vijavyo, kupitia mafundisho ya Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama, nao wanaiadhimisha.
Mfalme akatoa agizo hili kwa watu wote: “Adhimisheni Pasaka kwa BWANA Mungu wenu, kama ilivyoandikwa katika Kitabu hiki cha Agano.” . . .
Kabla wala baada ya Mfalme Yosia hapakuwepo na mfalme mwingine yeyote ambaye alimpenda BWANA kwa moyo wake wote, kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, sawasawa na Sheria yote ya Musa.
2 Wafalme 23:21–25
Akajibu, “Nendeni kwa mtu fulani huko mjini, mkamwambie, ‘Mwalimu asema hivi: Saa yangu imekaribia. Nitaiadhimisha Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.’ ”
Hivyo wanafunzi wakafanya kama vile Yesu alivyokuwa amewaelekeza, nao wakaandaa Pasaka.
Mathayo 26:18–19
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha