Waisraeli walipoingia Bahari ya Shamu walimwakilisha Yesu Akiingia kaburini, na Waisraeli kuvuka upande wa pili wa Bahari ya Shamu kulikuwa unabii wa ufufuo wa Yesu.
Mungu Alianzisha Siku ya Malimbuko katika Agano la Kale ili kwamba tusisahau kazi hii.
Kama vile Siku ya Malimbuko ilivyoadhimishwa katika Jumapili ya kwanza ifuatayo Pasaka na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu katika Agano la Kale, ufufuo wa Yesu, ambaye ni tunda la kwanza la wale waliolala, pia ulitokea siku ya Jumapili.
Matokeo yake, watakatifu wa Kanisa la mapema walikuja kushikilia imani kwamba hata kama wakifa, wataishi tena, na sikuzote walipata shangwe katika kuhubiri habari za wokovu, wakisimama upande wa Mungu.
Lakini kweli Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, tunda la kwanza la wale wote waliolala.
1 Wakorintho 15:20
Wakati huo huo pazia la Hekalu likachanika vipande viwili, kuanzia juu hadi chini. Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka.
Makaburi yakafunguka na miili ya watakatifu waliokuwa wamekufa ikafufuliwa.
Wakatoka makaburini, na baada ya Yesu kufufuka, waliingia kwenye Mji Mtakatifu na kuwatokea watu wengi.
Mathayo 27:51–53
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha